Ratiba ya mechi 4 za robo fainali imekamilika baada ya kumalizika kwa michuano ya raundi 16 bora mapema leo.
Baada ya mapumziko ya kesho kwota fainali zitaanza Ijumaa Fluminense kutoka Brazil wakimenyana na Al Hilal kutoka Saudia Arabia.
Mapema Jumamosi Palmeiras ya Brazil itakuwa na miadi dhidi ya Chelsea kutoka Uingereza huku mabingwa wa Ulaya PSG wapimane nguvu na Bayern Munich.
Borusia Dortmund ya Ujerumani itahitimisha ratiba na Real Madrid Jumamosi usiku.