Boniface Kariuki afariki akipokea matibabu Kenyatta

Maafisa wawili wa polisi waliohusika kwa mauaji hayo wangali wanazuiliwa korokoroni huku uchunguzi ukiendelea.

Dismas Otuke
1 Min Read

Boniface Mwangi Kariuki,mchuuzi wa barakoa aliyepigwa risasi kwa karibu na polisi wakati wa maandamano ya Juni 17 amefariki.

Kwa mjibu wa msemaji wa familia hiyo-Emily Wanjira ,Kariuki aliaga dunia mida saa tisa na robo alasiri.

Marehemu alikuwa amelazwa katika sadaruki ya hospitali kuu ya Kenyatta tangu Juni 17, alipolazwa baada ya kupigwa risasi katika barabara ya Moi kati kati ya jiji la Nairobi.

Madaktari walikiri kuwa ubongo wa marehemu uliacha kufanya kazi  punde alipowasilishwa hospitalini na kuondolea mbali uwezekaano wa kupona.

Maafisa wawili wa polisi waliohusika kwa mauaji hayo wangali wanazuiliwa korokoroni huku uchunguzi ukiendelea.

Kifo hicho kimejiri siku moja baada ya familia kuwataka wahisani waingilie kati ili kuwawezesha kulipia gharama ya matibabu iliyokuwa takriban shilingi milioni 3.5.

Share This Article