Mamlaka ya ushuru nchini (KRA),imeongeza muda wa kujaza fomu za kuthibitisha kulipa ushuru kwa siku moja hadi Julai mosi.
Kulingana na taarifa ya KRA muda mpya wa makataa ya kukamilisha zoezi hilo ni usiku wa manane wa Julai mosi.
Makataa ya awali ya kujaza fomu za ulipaji ushuru yalikuwa Juni 30 usiku wa manane.
Hatua hiyo inalenga kuwapa watu ambao hawashiriki zoezi hilo kulikamilisha.
Watakaokosa kujaza fomu hizo kufikia kesho usiku wa manane watapigwa faini ya shilingi 2,000 au asilimia tano ya ushuru wanaopaswa kudhihirisha.