Wabunge wa EALA wamtaka Ruto kuitisha kikao cha Marais kujadili uchechefu wa pesa

Dismas Otuke
1 Min Read

Wabunge wa Bunge la Afrika  Mashariki  EALA, wamemtaka mwenyeki wa Jumuiya ya EAC  Rais William Ruto, kuitisha kikao cha Marais, kujadili ukosefu wa fedha ambao umelemaza shughuli za bunge  hilo.

Kupitia kikao cha mtandaoni wakati wa kupitisha bajeti ya mwaka 2025 na 2026, wabunge hao wameapa kutolegeza kamba hadi kamati tekelezi ya bunge hilo itakapopokea pesa za kuendesha shughuli.

Shughuli nyingi za Bunge hilo zimekwama kutokana na uhaba wa pesa.

Share This Article