Washukiwa wa wizi Nyandarua, wakati wa maandamano wanaswa

Washukiwa hao wamewekwa korokoroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa Polisi wamewakamata washukiwa 11 wa wizi wa bidhaa wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z, Juni 25.

Polisi wameendesha msakao katika mitaa ya Huruma na Vatican mjini Ol’Kalou, mapema leo na kuwatia mbaroni washukiwa hao ambao pia walipatikana na baadhi ya mali ya wizi.

Washukiwa hao wamewekwa korokoroni wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Aidha baadhi ya bidhaa zilizoibwa na washukiwa hao zimepatikana, huku polisi wakiwataka wananchi kutoa taarifa kuhusu wahusika wa ghasia na fujo na uporaji  na uharibifu wa mali wakati wa maandamano hayo

Share This Article