Uharibifu wa vituo vya serikali wakashifiwa vikali

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali yalaani uharibifu wa miundomsingi wakati wa maandamanao.

Katibu wa idara ya uhamiaji na utoaji huduma kwa jamii Dkt. Belio Kipsang, amelaani uharibifu wa vifaa muhimu vya serikali ikiwa ni pamoja na kituo cha kitaifa cha usajili, katika majengo ya Naibu Kamishna wa kaunti ya Nyandarua wakati wa maandamano ya Gen Z Jumatano 25,2025.

Ghasia hizo zilisababisha uharibifu wa zaidi ya vitambulisho vya taifa 1,000 pamoja na vifaa viwili vya usajili wa kielektroniki, hatua ambayo imehujumu utoaji huduma muhimu za serikali.

“Kushambulia kituo cha kitaifa cha usajili, ni kushambulia roho ya taifa,’ alidokeza Kipsang’

Hata hivyo, katibu huyo alitoa ahadi kwa umma kwamba vituo vya dharura vya usajili vitapelekewa katika eneo hilo, ili kuwasaidia waliopoteza vitambulisho.

Alihakikisha kujitolea kwa serikali kulinda takwimu na habari za kibinafsi za wananchi.

“Licha ya kuwa miundomsingi imharibiwa, serikali imeweka mikakati kuhakikisha ulinzi wa deta,” alisema katibu huyo.

Aidha aliwahimiza vijana wa Gen Z kutumia nguvu yao kujieleza kupitia mikakati iliyopo na kwa amani.

Share This Article