Ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano zilipangwa kisiasa, asema Rais Ruto

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto

Rais William Ruto amekashifu vikali ghasia na uharibifu uliozuka wakati wa maandamano yaliyozuka Juni 25,2025, akiyataja hatua za kuhujumu uchumi wa taifa hili.

Kiongozi huyo wa taifa aliwanyooshea mkono baadhi ya viongozi wa kisiasa kwa kuwatumia vibaya  vijana waliokuwa na nia njema.

Akizungumza Ijumaa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya biashara ndogo na zile za kadri, Rais Ruto alisikitikia  maisha iliyopotea,  uharibifu na wizi wa mali, ambapo pia baadhi ya biashara ziliteketezwa na kusambaratisha maisha ya watu.

“Walioathirika pakubwa ni wafanyabiashara ambao waliamka na kupata biashara zao zimaharibiwa, zingine zikiwa zimeporwa,” alisema Rais Ruto.

Huku akithibitisha kuwa haki ya kuandamana imelindwa kwenye katiba, Rais alisisitiza kuwa maandam,anao hayo yalitekwa na wahalifu waliokuwa na mwingilio wa kisiasa.

“Tunaheshimu haki ya kuandamana. Lakini yake tuliyoshuhudia sio maandamanao ya amani. Zilikuwa ghasia za kupangwa. Ilikuwa ni hujuma dhidi ya uchumi,” alidokeza Rais Ruto.

Alimwagiza Inspekta Jenerali wa Polisi na asasi zingine za uwsalama kuchunguza yaliyotokea Juni 25,2025 na kuchukua hatua mwafaka za kisheria.

TAGGED:
Share This Article