Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon, alikosa kuweka rekodi mpya ya Dunia ya kukimbia mbio za maili moja chini ya muda wa dakika nne.
Kwenye shindano hilo lililoandaliwa jana usiku jijini Paris Ufaransa, maarufu kama Breaking4, Kipyegon alikosa kuafikia muda huo kwa takriban sekunde sita,akitimka kwa dakika 4 sekunde 6.42 ,akiboresha rekodi yake ya dunia kwa dakika 1 na sekunde 22.
Bingwa huyo mara tatu wa Dunia alianza vizuri katika uwanja wa Charléty, akiwa na wapigaji kasi 13 ,11 wanaume na watatu wa kike.
Hata hivyo Kipyegon angali na imani ataafikia muda huo katika siku zijazo.