Chemining ashinda taji ya kitaifa mbio za mita 10,000

Chemining ambaye pia  ni bingwa wa magereza, alitawala mbio hizo na kukata utepe wa kwanza kwa dakika 31 sekunde 22.39.09,

Dismas Otuke
1 Min Read

Loice Chemining wa huduma za Magereza, ndiye  bingwa mpya wa mita
10,000, katika mashindano ya kitaifa ya riadha  yaliyoanza leo katika
uwanja wa Ulinzi Complex.

Chemining ambaye pia  ni bingwa wa magereza, alitawala mbio hizo na kukata
utepe wa kwanza kwa dakika 31 sekunde 22.39.09,akifuatwa na Cintia
Chepnge’no wa KDF kwa dakika 32 sekunde 22.44, huku Rebecca Mwangi wa
Magereza akihitimisha nafasi tatu bora.

Mary Nyaruai wa Police aliibuka mshindi wa mita 1500, kwa kutumia muda
wa dakika 4  sekunde  09.68, akifuatwa na bingwa wa zamani wa dunia
kwa chipukizi Teresia Gateri kutoka Central na  Vivian Kiprotich wa
KDF katika nafasi za pili na tatu mtaliwa.

Mashindano hayo yatakamilika Ijumaa ,yakiwa mashindano ya mwisho ya uwanjani msimu huu.

Share This Article