Kumezuka na vuta ni kuvute kuhusu mazishi ya aliyekuwa Rais wa Zambia Edgar Lungu, baada ya Mahakama Kuu ya Pretoria nchini Afrika Kusini, kusitisha mazishi ya kiongozi huyo yaliyokuwa yaandaliwe jana nchini Afrika Kusini.
Serikali ya Zambia ilienda mahakamani kutaka kusitishwa kwa mazishi hayo katika taifa la kigeni, badala yake ikitaka marehemu azikwe nchini Zambia.
Familia ya marehemu Lungu inataka azikwe mjini Pretoria, Afrika Kusini, kwani hadi kifo chake, Lungu alikuwa na uhusiano wa karibu na Rais wa sasa, Hakainde Hichilema.
Lungu alifariki akiwa na umri wa miaka 68 Juni 5, akipokea matibabu chini Afrika Kusini.
Ibada ya mazishi ilikuwa imeanza Jumatano kabla ya Mwanasheria Mkuu wa Zambia Mulilo Kabesha, kupewa kibali cha kusimamisha mazishi.
Marehemu Lungu alihudumu kama Rais wa Zambia kati ya mwaka 2015 na 2021.
Kesi hiyo imeratibiwa kusikizwa Agosti 4 mwaka huu.