Trump: Vita vya Iran na Israel vitasitishwa hivi karibuni

Tom Mathinji
1 Min Read
Donald Trump - Rais wa Marekani

Rais Donald Trump wa Amerika amesema kuwa hatua ya kusitishwa kwa mapigano kati ya Iran na Israel inatarajiwa kuanza kutekelezwa katika muda wa saa chache zijayo.

Hatahivyo maafisa wa Iran na wale Israel hawajathibitisha makubaliano hayo, ingawaje Iran imesema itasitisha mashambulizi yake ya makombora iwapo Israel itasitisha mashambulizi yake.

Taharuki ilitanda zaidi jana usiku huku Israel ikitekeleza mashambulizi makali mjini Tehran.Awali Iran ilikuwa imefyetua makombora dhidi ya kituo cha kijeshi cha Amerika cha Al Udeid nchini Qatar,kulipiza kisasi mashambulizi ya Amerika dhidi ya viwanda vyake vya kinuklia siku ya jumamosi.

Rais Trump alithibitisha kwamba hakuna majeraha yalioripotiwa miongoni mwa wanajeshi wa Amerika huko Qatar, huku akipuzilia mbali shambulizi hilo la Iran.

Qatar  alisema makombora hayo ya Iran yalikabiliwa vilivyo  huku ikikashifu vikali shambulizi hilo ambalo lilitokea siku mbili baada ya ndege za kivita za Amerika kushambulia viwanda vya kinuklia nchini Iran.

Share This Article