Kirsty Coventry wa Zimbabwe ameshika hatamu leo kuwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kutoka kwa Thomas Bach.
Coventry mwenye umri wa miaka 40 ndiye mwanamke wa kwanza kuongoza kamati ya IOC.
Mshindi huyo mara saba wa Olimpiki na waziri wa zamani wa michezo nchini Zimbabwe, alinyakuwa dhahabu za uogeleaji katika mota 200 backstroke, katika makala ya mwaka 2004 mjini Athens, Ugiriki na mjini Beijing,China mwaka 2008.
Coventry ndiye Rais mwenye umri mdogo zaidi kuchaguliwa kuongoza IOC.
Hafla ya kukabidhibiwa mamlaka kwa Coventry, imehudhuriwa na zaidi ya wageni 700 mjini Lausanne nchini Uswizi.