Mamlaka ya bima ya matibabu nchini SHA, imewaonya waajiri wanaochelewesha michango ya ya wafanyikazi na kuwa itawachukulia hatua za kisheria.
SHA imefichua kuwa waajiri hawajawasilisha shilingi bilioni 20 zilizokatwa kutoka kwa wafanyiakzi na waajiri wao.
Haya yamesemwa Jumatatu alasiri na Katibu wa huduma za matibabu Dkt.Ouma Oluga, alipozindua shughuli ya kuwatuma maafisa wa SHA, kuzungumza na waajiri ili kuwashurutisha kuwasilisha makato ya ya wafanyikazi.
Dkt.Oluga amesema kuwa takriban waajiri 44,000, hawajawasilisha pesa walizokata kutoka kutoka kwa mishahara ya wafanyikazi ambazo kwa pamoja ni shilingi bilioni 20 ,hali inayolemaza utoaji huduma.
Aidha Dkt.Oluga amesema kati ya waajiri 44,000, ambao hawajawasilisha makato ya SHA,12,900 ni wa kaunti ya Nairobi.
Wafanyikazi 53,000 ndio wanaowalisha malipo ya SHA kwa wakati ufaao.

Wakiandamana na afisa mkuu Dkt.Mercy Mwangangi,Oluga amesema katika kipindi cha miezi sita ijayo maafisa wa SHA watakuwa wakiwatembelea waajiri wote ambao hawajawalisha michango ya wafanyakazi ili kuwawezesha kupata huduma hospitalini.
SHA imetoa makataa ya tarehe 9 kila mwezi kuwasilisha michango ya wafanyikazi ili ilipe madeni kwa hospitali zinazotoa huduma.