Maafisa wa polisi wakijumuisha wale wa GSU na wale wa akiba- National Police Reservists (NPR) ,katika eneo la Marti kaunti ya Samburu, waliongoza oparesheni siku ya Jumamosi na kupata mifugo 59 waliokuwa wameibwa.
Polisi hao walianzisha msako kufuatia taarifa iliyoandikishwa kuhusu wizi wa mifugo.
Imebainika kuwa mifugo hao 59, waliibiwa kutoka maeneo ya Nchalai na Angata mjini Nanyuki.
Wezi hao wa mifugo waliokuwa wamejihami kwa bunduki za AK-47, na kulizuka makabiliano makali baina yao na polisi punde walipofumaniwa, kabla ya kuzidiwa na polisi na kutoroka.
Mifugo hao tayari wamerejeshewa wamiliki.