Mshindi wa nishani ya shaba ya Olimpiki Faith Cherotich,aliibuka mshindi kwa mara ya tatu akiweka muda wa kasi wa dakika 8 sekunde 53.37 katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji ,mkondo wa diamond League ulioandaliwa Ijumaa usiku jijini Paris,Ufaransa.
Bingwa wa zamani wa Olimpiki Peruth Chemutai wa Uganda, alimaliza wa pili kwa dakika 8 sekunde 54.41, huku Sembo Alemayew wa Ethiopia, akimaliza wa tatu kwa dakika 9 sekunde 1.22.
Nelly Chepchirchir alishinda mbio za 1500 kwa dakika 3 sekunde 57.02, mbele ya Sarah Healy wa Ireland, na Birke Haylom kutoka Ethiopia, waliochukua nafasi za pili na tatu mtawalia.
Phanuel Kipkosgei Koech aliandikisha rekodi mpya ya dunia ya mita 1500 kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 akitimka kwa dakika 3 sekunde 27.72,akimaliza wa pili .