Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire akamatwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Kiongozi wa upinzani nchini Rwanda Victoire Ingabire akamatwa

Idara ya Upelelezi ya Rwanda imemkamata kiongozi wa upinzani saa chache baada ya kufika mahakamani kutoa ushahidi wake katika kesi inayowakabili baadhi ya wafuasi wake wanaotuhumiwa kwa jaribio la kupindua mamlaka mjini Kigali.

Victoire Ingabire ametajwa katika kesi dhidi ya watu tisa ambao ni pamoja na mwandishi wa habari wa ndani, na baadhi ya wanachama wa chama chake.

Ingabire aliiambia Mahakama Kuu mjini Kigali Alhamisi asubuhi kwamba hakuhusika kivyovyote katika mafunzo ya mtandaoni ya 2021 yaliyotolewa kwa washtakiwa kupindua serikali kwa njia za amani, ambazo ni msingi wa mashtaka dhidi yao.

Jana jioni mahakama ilitangaza kuwa haikuridhika na ushahidi wake na kuamuru uchunguzi wa wiki mbili dhidi yake, kabla ya ofisi ya idara ya upelelezi kutangaza kukamatwa kwake katika taarifa ya X usiku wa manane.

Share This Article