Makundi ya kiufundi kutoka serikali za Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yametayarisha mwafaka wa kuleta amani mashariki mwa Congo .
Mwafaka huo unatarajiwa kutiwa saini Juni 27 na utashuhudia kukomeshwa kwa uhasama na mapigano mashariki mwa DRC,hususan eneo Goma lenye madini mengi.
Endapo hatimaye mwafaka huo utasainiwa itakuwa hatua kubwa kwa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kuwaunganisha marais Felix Tshisekedi wa RDC na Paul Kagame wa Rwanda kwa mara ya kwanza baada ya uhasama wa miongo kadhaa.
Makumi ya maefu ya watu wameangamia katika eneo la Goma, kufuatia makabiliano makali kati ya wanamgambo wa M23, waliodaiwa kuungwa mkono na Serikali ya Kagame na wanajeshi wa Tshisekedi.