Rais Ruto: Lazima tufaulu

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amerejelea kujitolea kwa serikali yake kuimarisha uchumi wa taifa hili, akiwahimiza viongozi kutolegeza kamba katika kutimiza ahadi zilizotolewa kwa Wakenya.

Akizungumza Alhamisi wakati wa  mkutano wa tatu wa Baraza la Mawaziri na utathimini wa kipindi cha nusu ya muhula, katika taasisi ya uongozi ya KCB Karen Nairobi, kiongozi wa taifa alitambua changamoto zinazoghubika nchi hii, lakini akadokeza kuwa hatua za kijasiri zilizochukuliwa na utawala wake, zimeanza kuzaa matunda.

“Safari ya kuimarisha uchumi wa taifa hili imekumbwa na changamoto si haba, hatua iliyotusababisha kuchukua hatua za kijasiri. Hata hivyo hatua hizo zimeanza kuzaa matunda,” alisema Rais Ruto.

Mkutano huo wa siku mbili unalenga kutathmini utekelezaji wa Ajenda ya kuimarisha Uchumi kutoka chini almaarufu  (BETA), kwa kuangazia sekta muhimu za uchumi wa taifa hili.

Kiongozi wa taifa alielezea matarajio waliyonayo wakenya na umuhimu wa umoja katika uongozi.

“Hatupasi kufeli. Tusipofaulu tutakuwa tumedidimiza matumaini ya taifa hili,” aliongeza Rais Ruto.

Mkutano huo utakaokamilika Ijumaa, unahudhuriwa na Rais William Ruto, Naibu  Rais Kithure Kindiki, Mawaziri, Makatibu wa wizara, na maafisa wengine wakuu serikalini.

TAGGED:
Share This Article