Starlets walenga ushindi mnono dhidi ya Sudan Kusini michuano ya CECAFA

Dismas Otuke
1 Min Read

Vidosho wa kenya Harambee Starlets,watalenga ushindi mkubwa leo jioni watakapochuana na limbukeni Sudan Kusini kwenye mashindano ya kombe la CECAFA, uwanjani Azam Complex jijini Dares Salaam,Tanzania.

Kenya waliichabanga Burundi magoli 3-0, katika mchuano wa ufunguzi, kabla ya kuwanyofoa mabingwa watetezi Uganda, mabao 4-0, katika mechi ya pili.

Starlets wameratibiwa kuchuana na wenyeji Twiga Stars, Jumamosi hii katika mchuano utakaobaini mabingwa wa mwaka huu.

Tanzania watamenyana na Uganda katika mchuano wa kwanza kuanzia saa kumi jioni.

Share This Article