Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Lagat kufika mbele ya IPOA Alhamisi

Aidha Hassan alikariri kuwa hakuna yeyote atakayepatikana na hatia atakayesazwa kwenye kesi hiyo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Naibu Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi Eliud Lagat, anatarajiwa kufika mbele ya Mamlaka Huru ya kusimamia Utendakazi wa Polisi IPOA, leo Alhamisi Juni 19, 2025, kuandikisha taarifa kuhusiana na mauaji ya Mwanablogu Albert Ojwang.

Mwenyekiti wa IPOA Isaac Hassan, alisema wamemwita Lagat kufika mbele ya IPOA, kwani alikuwa mlalamishi mkuu kwenye kesi ya marehemu Ojwang.

Aidha, Hassan alikariri kuwa hakuna yeyote atakayepatikana na hatia atakayesazwa kwenye kesi hiyo.

Marehemu Ojwang, alifarki katika hali tatanishi mikononi mwa polisi wa kituo cha Central mapema mwezi huu.

Share This Article