Afisa wa polisi akamatwa kwa kumpiga risasi raia Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanha.

Afisa wa polisi ametiwa nguvuni kwa kumpiga risasi mtu anayedaiwa kuwa mchuuzi wakati wa maandamano katikati mwa Jiji la Nairobi.

Kupitia kwa taarifa, Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS) imesema kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi ameagiza afisa huyo akamatwe mara moja, baada ya kumjeruhi mchuuzi huyo kwa kumpiga risasi.

Msemaji wa polisi Muchiri Nyaga, alisema kuwa mwathiriwa huyo anaendelea kupokea matibabu hospitalini, akidokeza kuwa NPS inakashifu vikali hatua hiyo ya afisa huyo wa polisi.

Wakati huo huo Huduma hiyo ya Polisi ilisema imeshuhudia baadhi ya watu waliokuwa na silaha wakati wa maandamano hayo na imeanzisha uchunguzi kuwachukulia hatua za kisheria.

“Huduma ya Taifa ya Polisi haiungi mkono kwa vyovyote hatua ya kubuniwa kwa makundi hayo. Watu hao watachukuliwa hatua za kisheria. Uchunguzi umeanzishwa kuwakamata wahalifu,” alisema Nyaga kwenye taarifa.

Share This Article