Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets itashuka uwanjani Azam Complex, kesho jioni jijini Dares Salaam,Tanzania kwa mchuano ufunguzi wa makala ya mwaka huu ya michuano ya CECAFA.
Starlets wanaofunzwa na Beldine Odemba, wamefanya mazoezi ya mwisho leo jioni huku wakitumia mashindano hayo kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Gambia mwezi Oktoba mwaka huu.
Burundi walioshinda bao moja kwa bila dhidi ya Uganda siku ya Ijumaa ,watalenga ushindi wa pili dhidi ya Kenya .
Wenyeji Tanzania walisajili ushindi mkubwa wa magoli 4-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mechi ya ufunguzi.