Waliohusika na mauaji ya Ojwang wataadhibiwa, asema Mwaura

Tom Mathinji
1 Min Read
Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura.

Hatibu wa serikali Isaac Mwaura, amewataka Wakenya kuwa utulivu huku uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kifo cha mwanablogu mwalimu Albert Ojwang.

Mwaura alihakikishia umma kwamba serikali kupitia kwa Halmashauri Huru ya Kutadhmini Utendakazi wa Polisi (IPOA), imejitolea kuhakikisha wahusika wa mauaji hayo wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu, Mwaura alikariri msimamo wa Rais William Ruto kuhusu suala hilo na akaomba wanasiasa wasiingize siasa kwenye suala hilo.

Alilaani maandamano ya hapo juzi jijini Nairobi yaliyosababiksha uharibufu wa mali akiwataka wanachi kuelezea malalamiko yao kwa njia ya mazungumzo.

Mwaura aidha alipuzilia mbali madai ya siku kuu ya kitaifa tarehe 25 mwezi huu, akionya vijana dhidi ya kueneza habari potovu.

Alisema Mswaada wa Fedha wa mwaka 2025/2026 umewajali wananchi, ukilenga kubuni ajira kwa vijana na kwamba hakuna ushuru mpya ulioanzishwa.

TAGGED:
Share This Article