Rachel Ruto: Tusiwatenge walemavu

Tom Mathinji
1 Min Read
Mama Taifa Rachel Ruto akiwakumbatia watoto walio na ulemavu wa ngozi.

Mama Taifa Rachel Ruto, ametoa wito kwa jamii kudumisha mazingira yanayowakumbatia wanaoishi na ulemavu.

Alisema heshima ya taifa hudhihirishwa pakubwa na fursa zinazotolewa kwa wale walio na mahitaji maalum.

Aliyasema hayo Ijumaa alipoongoza sherehe za kuadhimisha siku ya Kimataifa ya uhamasishaji kuhusu ulemavu wa ngozi, iliyoandaliwa katika uwanja wa Huruma, Eldoret Kaunti ya Uasin Gishu.

“Katika mazingira ambapo kila mmoja anakubalika, tunaweza hakikisha kila mmoja bila kuzingatia maumbile yake, anapewa haeshima anayohitaji,” alisema Mama Taifa.

Alidokeza kuwa watu walio na ulemavu wa ngozi, husababisha mchango mkubwa katika jamii.

“Wana talanta za kupigiwa mfano,na uwezo unaodhihirisha tamaduni tofauti. Kwa kutambua na kukubali mchango wao, tunaimarisha uwezo wa kuwa sehemu ya jamii,’ aliongeza Mama Taifa.

Aidha aliwatambua na kuwapongeza wakenya ambao wamekabiliana na changamoto za ulemavu wa ngozi, akiwemo Msemaji wa Serikali Isaac Mwaura na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Grace Mumbi Ngugi.

TAGGED:
Share This Article