Afisa msimamizi wa kituo cha polisi cha Central kaunti ya Nairobi Samson Talaam, amekamatwa na Polisi mjini Eldoret kwa kushukiwa kuhusika kwenye mauji ya Mwanablogu na Mwalimu Albert Ojwang’.
Talaam alikuwa amesimamishwa kazi kufuatia kufariki kwa Ojwang’ akiwa kwenye seli ya Central .
Kulingana na ripoti za Polisi, maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), walimkamata Talaam, baada ya kumsaka kwa takriban siku mbili bila mafanikio.
Ojwang’ aliripotiwa kufariki Juni 8,2025 katika hali ya kutatanisha huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo cha mauji hayo ya kinyama na wahusika wakuu.
Haya yanajiri wakati ripoti ya Hospitali ya Mbagathi, aliporitiwa kupelekwa marehemu kwa matibabu usiku wa Juni 7,kukinzana na ripoti ya awali ya polisi.
Hospitali hiyo imesema marehemu aliwasilishwa hospitalini humo mida ya saa nane usiku wa manane akiwa tayari amefariki.
Awali Polisi wa Central walitoa taarifa kuwa marehemu alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kupatikana akiwa mahututi gerezani.