Afisa wa polisi Constable James Mukhwana, aliyekuwa zamuni akisimamia seli katika kituo cha polisi cha Central wakati Albert Ojwang alifikishwa kwenye kituo hicho, ametiwa mbaroni na atashtakiwa kwa mauaji.
Kulingana na ripoti kutoka kituo cha polisi cha Capitol Hill, Mukhwana alikamatwa Alhamisi na maafisa kutoka kitengo cha kushughulikia maswala ya ndani cha Huduma ya Taifa ya Polisi (IAU) na wale wa Halmashauri Huru ya Kutathmini Utendakazi wa polisi (IPOA).
Kwa sasa afisa huyo anazuiliwa katika kiuo cha polisi cha Capitol Hill, Jijini Nairobi.
“Atafunguliwa mashtaka ya mauaji kuambatana na sehemu ya 203 na ile ya 204 ya katiba, kufuatia kifo cha Albert Ojwang. IPOA na IAU zinatekeleza haya. Habari zaidi zitatolewa baadaye,are dealing. More details to follow,” ilisema taarifa kutoka kituo cha polisi cha Capitol Hill.