Vitengo vya Usalama hapa nchini, vimetengewa shilingi bilioni 464.9 kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026 iliyosomwa leo Alhamisi kwenye majengo ya bunge.
Akiwasilisha bajeti hiyo, waziri wa Fedha John Mbadi,alisema mgao huo ni nyongeza ya shilling billion 87.4 kutoka shilling billion 377.5 zilizokuwa zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka 2024/2025.
Vikosi vya Ulinzi (KDF) vimetengewa shilingi bilioni 202.3, Huduma ya Taifa ya polisi (NPS) shilingi bilioni 125.7, shilingi bilioni 51.4 zikitengewa idara ya Ujasusi wa Taifa (NIS), shilingi bilioni 32.5 kwa wizara ya Usalama wa Taifa na shilingi bilioni 38.1 zikitengewa Idara ya Magereza.
Waziri Mbadi alipendekeza shilingi bilioni 10 zitakazotumiwa kwa ukodeshaji wa magari ya polisi na shilingi zingine bilioni 3.6 kwa mipango ya Huduma ya Taifa ya Polisi.
Maudhui ya bajeti ya mwaka huu ni ufufuzi endelevu wa kiuchumi kwa maisha bora,kubuni nafasi za ajira,ukuzi wa biashara na ustawi wa viwanda kuambatana na ajenda ya serikali ya mageuzi ya kiuchumi.