Rais William Ruto amesema taifa hili litabadilishwa na viongozi watakaochukua hatua za kijasiri kuimarisha maisha ya wananchi wote.
Akizungumza Jumatatu aliposhiriki meza ya mazungumzo na wasanii wa hapa nchini, kiongozi wa taifa alisema maamuzi dhabiti yaliyochukuliwa na serikali, yamesababisha kuimarika kwa uchumi wa taifa hili, kupitia ongezeko la uzalishaji wa bidhaa za kilimo na kuboresha usalama wa kijamii.
Kiongozi wa taifa alisema kuwa walichukua hatua mwafaka, kufanikisha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu pamoja na kuhakikisha wakenya wanapata huduma bora za afya ambazo ni nafuu.
Alidokeza kuwa katika mkutano huo na wasanii hao, walikubaliana kushirikiana kuhakikisha Kenya linakuwa taifa bora kwa wote.