Watu sita wafariki kwenye ajali ya barabarani Nyandarua

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamume awaua wanawe wawili kabla ya kujitoa uhai Mai Mahiu.

Watu sita wamefariki kwenye ajali ya barabarani katika barabara ya Ol Jororok–Nakuru. 

Miongoni mwa wale walioangamia kwenye ajali hiyo ni wanaume wanne, mwanamke mmoja na mtoto wanaoaminika kuwa watalii. Watu wengine 27 walipata majeraha na walipelekwa hospitalini wakiwa hali mahututi.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamishna wa kaunti ya Nyandarua Abdlisack Jardesa, alisema kundi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Nakuru kueleleka katika hoteli ya Panari mjini  Nyahururu kwa malazi kabla ya kuendelea na safari yao.

Gari lao linaaminika lilipoteza mwelekeo, kabla ya kubingiria na kuanguka kwenye shimo katika eneo la Gichaka.

“Tumethibitisha kuwa watu sita wamefariki kwenye ajali hii. Hata hivyo tunachunguza kubaini uraia wao. Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya Nyahururu kwa matibabu,” alisema Jadesa.

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, basi hilo lilipoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa wakati mvua ilipoanza kunyesha mwendo wa saa kumi alasiri.

“Lilipoteza mwelekeo na kubingiria. Kisha liligonga mti na kusimama. Tulifika hapo kuwaokoa abiria,” alisema tMacDavis Wanjau, aliyeshuhudia ajali hiyo.

TAGGED:
Share This Article