Hatuchezi na Simba ng’oo ,Yanga wasimama kidete

Wakiwa wamecheza mechi 27 zikisalia mechi tatu msimu ukamilike, Yanga wangali kuongoza jedwali kwa pointi 73, alama moja zaidi ya Yanga, huku timu zote zikifuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uongozi wa Klabu ya Young Africans umeweka bayana kuwa kamwe hautashiriki katika mechi namba 184 ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba SC, ikiwa derby ya Kariakoo, iliyopangwa kupigwa Jumamosi hii Juni 15, 2025, hadi matakwa yao yatakapotekelezwa.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa leo Juni 9, 2025, klabu hiyo imethibitisha kuhudhuria kikao maalum kilichoitishwa na Bodi ya Ligi Kuu kujadili mustakabali wa mchezo huo, ambapo waliwasilisha msimamo wao kwa maandiko.

Yanga imeeleza kuwa uamuzi wao unalenga kulinda maendeleo ya soka nchini, na imeitakia heri Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi katika kushughulikia hoja walizowasilisha.

Wakiwa wamecheza mechi 27 zikisalia mechi tatu msimu ukamilike, Yanga wangali kuongoza jedwali kwa pointi 73, alama moja zaidi ya Yanga, huku timu zote zikifuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Share This Article