Bibiani Gold Stars washinda Ligi Kuu Ghana kwa mara ya kwanza

Timu hiyo ilipandishwa ngazi kushiriki Ligi Kuu mwaka 2021 kwa mara ya kwanza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bibiani Gold Stars FC, ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ghana,  kwa mara ya kwanza baada ya kusajili ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Accra Lions, jana katika mechi ya kufunga msimu.

Ushindi huo uliwapa Gold Stars FC, tiketi ya kushiriki kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika msimu ujao.

Bibiani  Gold Stars walikamilisha msimu kwa pointi 63 ,alama tatu zadi ya Nations FC  na Heart of Lions, waliomaliza katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

Timu hiyo ilipandishwa ngazi kushiriki Ligi Kuu mwaka 2021 kwa mara ya kwanza.

Share This Article