Majaribio ya kitaifa kuteua kikosi cha Kenya kitakachoshiriki mashindano ya Riadha Duniani yataandaliwa baina ya Agosti mosi na mbili mwaka huu jijini Nairobi.
Awali majaribio hayo yalikuwa yameratibiwa kati ya Julai 26 na 27 .
Chama cha riadha Kenya kimesisitiza kuwa wanariadha wote watakaoalikwa kwa majaribio hayo ya siku mbili; ni sharti wawe wametimiza muda wa kufuzu na pia kuafiki viwango vya kupimwa dhidi ya ulaji muku.
Wanariadha watakaoteuliwa wataripoti kambini huku wale wa mbio za masafa mafupi wakikita kambi mjini Marseille, Ufaransa, katika kambi ya Miramas.
Mashindano ya Riadha Duniani Makala ya 20, yataandaliwa jijini Tokyo, Japan, kuanzia Septemba 13 hadi 21 mwaka huu.