Mwigizaji tajika wa Nigeria Iyabo Ojo amemtetea binti yake Priscilla ambaye ameolewa hivi maajuzi na mwanamuziki wa Tanzania Juma Jux dhidi ya shutuma za Mange Kimambi.
Hii ni baada ya Mange kukashifu maudhui ya wanandoa hao wawili mitandaoni akisema kwamba yanalenga kuondoa fikra za raia wa Tanzania kwenye mambo muhimu yanayowahusu kisiasa ili wawaangazie.
“Nimeshtushwa na ujasiri wako! Kurejelea mwanangu na mume wake kwa namna hiyo, kurejelea maudhui yao kuwa ya kijinga, kujaribu kueneza woga, haikubaliki” alisema Iyabo katika chapisho lake la kumjibu Mange Kimambi.
Mama huyo aliendelea kuelezea jinsi alimlea binti yake akisema kwamba yeye na mume wake ni watu wa amani lakini yeye hachezi na yeyote anayejaribu kuingilia binti yake.
Alifafanua kwamba madai ya Mange Kimambi kwamba serikali ya Tanzania ilifadhili harusi ya Priscilla na Jux sio ya kweli na kwamba kulingana na tamaduni za Nigeria, familia ya bi harusi hugharamia harusi.
Huku akifichua kwamba yeye pia ni mwanaharakati, Iyabo Ojo alimwambia Mange kwamba uongozi wa kweli unahitaji uwepo na moyo akishangaa jinsi yeye anayeishi nchini Marekani anataka kuamuru jinsi Prissy na Jux wataishi maisha yao nchini Tanzania.
“Toa binti yangu kwenye harakati zao. Atachapisha akipendacho, wakati apendao na jinsi apendavyo. Hahitaji mapenzi yako, anapenda sana ipasavyo” alimalizia Iyabo akisema kwamba daima atalinda watu wake.
Mange alikuwa amechapisha ujumbe kwenye Instagram uliomlenga Priscilla akimtaka yeye na Jux waache kuchapisha yanayowahusu mitandaoni na kupotosha watazania kutoka kwa mambo muhimu hasa uchaguzi.
Aligusia onyesho la wawili hao linalotarajiwa kuandaliwa jijini London nchini Uingereza Juni 13, 2025 akisema nayo inalenga kuendeleza upotoshaji huo.
Kimambi alimtaja pia Diamond Platnumz ambaye pia alimtaka akomeshe sarakasi za maisha yake mpaka uchaguzi ukmilike.