Timu ya taifa ya soka Harambee Stars, itashuka uwanjani Marrakech nchini Morocco, kwa mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Chad, kuanzia saa kumi na mbili leo jioni.
Kenya inatumia mchuano huo kujiandaa kwa makala ya nane ya fainali za CHAN, zitakazoandaliwa na Kenya, Uganda na Tanzania kuanzia Agosti 2 mwaka huu.
Kenya ni ya 111 katika msimamo wa Dunia wa FIFA huku Chad, ikishikilia nafasi ya 177 .
Timu hizo zinakutana kwa mara ya kwanza leo, kabla ya kumenyana tena Jumanne ijayo.