Washukiwa wawili wamekamatwa wakisafirisha pembe sita za ndovu kwenye barabara ya Lodwar-Kalokol, kaunti ya Turkana.
Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Turkana ya kati Evans Ombui, alisema wawili hao walikamatwa baada polisi kupashwa habari na wananchi.
Pembe hizo zina uzani wa kilo 26.4, kulingana na Afisa Mkuu wa Huduma ya Taifa kwa Wanyamapori (KWS) kaunti ya Turkana, Elijah Chege.
‘Wananchi waliwajulisha maafisa wa KWS, ambao waliwahusisha maafisa wengine wa usalama na kuwatia nguvuni washukiwa hao katika eneo la Monti takriban kilomita 45 kutoka mji wa Lodwar ,’ alisema Ombui.
Washukiwa hao watafikishwa mahakamani Jumatatu.