KPC na GSU wanusia ubingwa wa Ligi Kuu Voliboli

 General Service Unit waliiparamia Kenya Ports Authority seti tatu kavu za 25-15, 25-22, 30-28.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara tano wa Afrika katika Voliboli ya wanawake Kenya Pipeline (KPC) wameisasambua DCI seti 3-0, katika mkumbo wa kwanza wa fainali ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu KVF uliosakatwa Ijumaa katika ukumbi wa Kasarani .

KPC wamesajili ushindi wa seti za 25-19, 25-20, na 25-14, katika fainali ya kwanza huku wakinusia taji hiyo waliyopata kwa Kenya Commercial Bank mwaka jana.

KPC watatawazwa mabingwa endapo watashinda marudio ya fainali dhidi ya DCI kesho.

General Service Unit waliiparamia Kenya Ports Authority seti tatu kavu za 25-15, 25-22, 30-28.

GSU wanawania ubingwa wa ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022 na la 16 kwa jumla.

Share This Article