Wakenya wasihahe licha ya uhaba wa chanjo asema Oluga

Dkt. Oluga amekiriwa kuwa kaunti 12 kati ya 47 nchini zina upungufu wa chanjo

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakenya wametakiwa kutokuwa na wasiwasi licha ya kuripotiwa kwa upungufu mkubwa wa chanjo za Polio,Rotavirus na BCG nchini.

Katibu wa huduma za matibabu Dkt. Ouma Oluga, amesema tayari imepokea chanjo milioni 3.2 za Polio, na nyingine milioni 3 za BCG, zinatarajiwa kuwasili kufikia Juni 10 na 15 mtawalia  mwaka huu.

Hii ni baada ya Wizara ya Afya kupitia kwa taarifa yake Oluga, kukiri kuwepo kwa upungufu mkubwa wa chanjo humu nchini.

Dkt. Oluga amekiriwa kuwa  kaunti 12 kati ya 47 nchini zina upungufu wa chanjo, ambapo chanjo za BCG na Polio, zimesalia zile za matumizi kwa wiki mbili huku kiwango cha chanjo ya Rotavirus kikisalia cha matumizi ya mwezi mmoja pekee.

Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuainisha ugavi upya wa chanjo zilizosalia ili kuwa na usawa.

Share This Article