Uhispania wanusurika mikononi mwa Ufaransa,wafuzu fainali ya UEFA Nations League

Uhispania watapimana ubabe na Ureno katika fainali ya Jumapili hii ugani Allianz nchini Ujerumani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa kombe la UEFA Nations League, Uhispania, waliponea chupuchupu waliposajili ushindi wa mabao 5-4 katika nusu fainali ya pili, iliyosakatwa jana usiku mjini Stuttgart, Ujerumani.

Lamine Yamal alipachika mabao mawili kwa Uhispania huku Mikel Merino, Nico Williams na Pedri wakifunga bao moja kila mmoja .

Ufaransa walifunga yao manne kupitia kwa Kylian Mbappe, Kolo Mauani na Rayan Cherki, huku Dani Vivian akijifunga moja.

Uhispania watapimana ubabe na Ureno katika fainali ya Jumapili hii ugani Allianz nchini Ujerumani.

Ureno walifuzu kwa fainali baada ya kuwakwatua wenyeji Ujerumani mabao 2-1.

Uhispania wanalenga kunyakua kombe la tatu la Ulaya, baada ya kutwaa kombe la Euro na UEFA Nations League msimu wa mwaka 2022/2023 na kunyakua kombe la UEFA Euro mwaka jana.

Share This Article