Mabingwa wa Ligi Kuu ya mpira wa wavu kwa wanaume na wanawake wanatarajiwa kubainika baina ya Ijumaa Juni 6 na Jumamosi Juni 7,wakati wa mechi za fainali katika ukumbi wa Kasarani.
KPC watafungua ratiba kwa kuvaana na limbukeni DCI katika upande wa wanawake kuanzia saa nane, kabla ya kupisha GSU kuvaana na KPA kwa mechi ya wanaume.
Jumamosi kutapigwa mechi nne za mwisho Kenya Prisons wakichuana na KCB,DCI wapimane nguvu na KPC huku GSU wakihitimisha ratiba dhidi ya KPA kwa wanawawake.
Upande wa wanaume utashuhudia Equity wakiwa na miadi Kenya Prisons.