Mataifa 10 ya Afrika yawekewa vikwazo vya usafiri na Marekani

Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa Jumatatu  usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais wa Marekani Donald Trump.

Nchi 10 za Afrika ni miongoni mwa 12 zilizowekewa vikwazo vya usafiriki na Marekani kuanzia Jumatatu ijayo.

Taarifa iliyotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatano, ilisema raia wa mataifa yaliyopigwa marufuku hawataruhusiwa kuingia Marekani.

Mataifa yaliyofungiwa kuingia Marekani kutoka Afrika ni; Chad, Somalia, Congo, Equatorial Guinea, Eritrea, Libya na Sudan.

Nchi zilizowekewa vikwazo kiasi bila kufungiwa ni Burundi, Sierra Leone na Togo.

Mataifa mengine yaliyopigwa marufuku ni Afghanistan, Myanmar, Haiti, Iran, na Yemen.

Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa Jumatatu  usiku.

 

Share This Article