Trump apiga marufuku usajili wanafunzi wa kigeni katika chuo cha Harvard

Trump siku ya Jumatano alitaja kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa usajili wa wanafunzi wa kigeni chuoni humo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Donald Trump wa Marekani, amepiga marufuku usajili wa wanafunzi wapya wa kigeni katika chuo kikuu cha Harvard, kwa kipindi cha miezi sita.

Trump siku ya Jumatano alitaja kuwa tishio kwa usalama wa kitaifa usajili wa wanafunzi wa kigeni chuoni humo.

Upande wake usimamizi wa chuo cha Harvard, umetaja hatua hiyo kuwa isiyo na mashiko na kuapa kuendelea kulinda haki za wanafunzi wake wa kigeni.

Amri hiyo ya Trump, pia imesitisha mara moja utoaji wa Viza kwa wanafunzi wa kimataifa wanaotaka kujiunga na chuo hicho, huku pia akitafakari kuwapokonya Viza wanafunzi wanaondelea na masomo chuoni humo.

Share This Article