Waziri wa Utalii Rebecca Miano amekariri kujitolea kwa serikali kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa katika kaunti ya Nyandarua.
Miano alisema haya Jumatatu alipohudhuria mazishi ya Mama Jane Wangari eneo bunge la Ndaragwa, akisisitiza kuwa miradi hiyo itainua hadhi ya wakazi wa Nyandarua itakapokamilika.
Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa masoko ya kisasa, upatikanaji wa maji safi, uunganishaji wa umeme na kuboresha taasisi za elimu na vituo vya afya.