Kazi mtaani kurejea kote nchini kuanzia wiki ijayo

Katika mradi wa Kazi Mtaani vijana hushirikishwa kwa kazi za usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi na kupokea malipo kila wiki.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mradi wa ajira kwa vijana wa Kazi Mtaani, utaanzishwa kote nchini kuanzia wiki ijayo asema Rais William Ruto.

Akitangaza hayo wakati wa sherehe za 62 za siku kuu ya Madaraka zilizoandaliwa uwanjani Raila Odinga ,kaunti ya Homa Bay,Rais William Ruto alisema kuwa vijana 110,000 watashirikishwa.

Mradi huo ulikuwa umeanzishwa na utawala uliopitwa  wakati wa janga la Corona, kabla ya kusitishwa punde baada ya Rais Ruto kutwaa mamlaka.

Katika mradi wa Kazi Mtaani vijana hushirikishwa kwa kazi za usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi na kupokea malipo kila wiki.

Share This Article