Watu 151 wafariki kwenye mafuriko Nigeria

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 151 wafariki kwenye mafuriko Nigeria.

Takriban watu 151 wamefariki kutokana na mafuriko, huku maelfu ya wengine wakihama makwao katika eneo la Niger, nchini Nigeria.

Mkurugenzi wa Habari katika shirika la Kushughulikia maswala ya dharura katika jimbo la Niger Ibrahim Audu Hussaini, alithibitisha idadi hiyo, akiongeza kuwa makundi ya uokoaji yanaendelea kutafuta miili zaidi.

Kulingana na Hussaini, zaidi ya familia  500 zimeathiriwa na zaidi ya watu 3,000 wamelazimika kuhama makazi yao.

Tukio la mafuriko katika mji wa kati wa Mokwa katika Jimbo la Niger lilitokea Jumatano usiku na kuendelea hadi Alhamisi asubuhi.

Siku kadhaa baadaye, waokoaji walikuwa wakiendelea kutafuta miili katika vifusi.Nigeria inakabiliwa na mafuriko wakati wa msimu wa mvua, ambao ulianza Aprili.

Mnamo mwaka wa 2022, wimbi baya zaidi la mafuriko nchini humo kuwahi kushuhudiwa katika zaidi ya muongo mmoja liliua zaidi ya watu 600, kuharibu makazi karibu milioni 1.4 na kuharibu zaidi ya ekari milioni 1 za mashamba.

TAGGED:
Share This Article