Mwenyekiti wa Raga nchini KRU, Sasha Mutai, ajiuzulu

 Mutai amejiuzulu leo kwenye mkutano mkuu maalum ulioandaliwa katika makao makuu ya KRU.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mwenyekiti wa chama cha raga nchini KRU, Sasha Mutai, amejiuzulu siku ya Ijumaa saa chache kabla ya kuwasilishwa kwa hoja ya kutokuwa na Imani naye.

Mutai amejiuzulu leo kwenye mkutano mkuu maalum ulioandaliwa katika makao makuu ya KRU.

Mutai anadaiwa kujihusisha na ufujaaji wa shilingi milioni 13.2, kwa malipo kwa watu ambao hawakutoa huduma.

Hoja ya kutaka kumtimua afisini Mutai ilikuwa iwasilishwe na Katibu wake Mkuu Ray Olendo, madai ambayo ameyakanusha kabla ya kujiuzulu.

Mutai alichaguliwa Mwenyekiti wa chama cha KRU bila kupingwa katika uchaguzi wa Machi 23 mwaka uliopita.

Kujiuzulu kwa Mutai kunajiri majuma matatu kabla ya uchaguzi wa kamati ya Olimpiki (NOCK), akiwania kiti cha mwanachama wa kamati kuu.

Share This Article