Serikali yajizatiti kupunguza gharama ya kutibu Saratani

Tom Mathinji
1 Min Read
Matibabu ya Saratani kupungua hapa nchini.

Ni afueni kwa wagonjwa wa Saratani ya matiti nchini, huku wakitarajiwa kunufaika kutokana na kupunguzwa pakubwa kwa gharama ya matibabu.

Gharama ya matibabu ya ugonjwa huo inatarajiwa kupungua kutoka shilingi 120,000 hadi shilingi 40,000, kufuatia ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na shirika la Roche East Africa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Waziri wa Afya  Aden Duale alisema hatua hiyo itaimarisha hali ya kifedha kwa wagonjwa wanaougua saratani, na kufanikisha ajenda ya taifa ya kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa wote. 

“Ushirikiano huu ni hatua kubwa katika kumarisha upatikanaji wa huduma nafuu za afya, matibabu ya ubora wa juu ya Saratani, hususan Saratani ya Matiti,” alisema Duale.

Kulingana na Duale ushirikiano huo utatekelezwa katika vituo vyote vilivyo na kandarasi ya Mamlaka ya Afya ya Jamii-SHA, ikiwa ni pamoja na hospitali za umma, za kidini na za kibinafsi—ili kuhakikisha upatikanaji sawa wa huduma.

Share This Article