Peter Ndegwa ateuliwa mwenyekiti wa Safricom Ethiopia

Safaricom inajivunia jumla ya wateja milioni 50 nchini Kenya na Ethiopia.

Dismas Otuke
0 Min Read

Bodi ya usimamizi ya kampuni ya Safaricom Ethiopia, imemteua Afisa Mkuu mtendaji Peter Ndegwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya Michael Joseph aliyestaafu.

Ndegwa, atahudumu kwa majukumu hayo mawili baada ya Joseph kuhudumu kwa bodi zote mbili za Safaricom Kenya na Safaricom Ethiopia kwa kipindi cha miaka minne iliyopita.

Safaricom inajivunia jumla ya wateja milioni 50 nchini Kenya na Ethiopia.

Share This Article