Julie na Todd Chrisley waachiliwa huru

Wawili hao walipatiwa msamaha na Rais Trump.

Marion Bosire
1 Min Read

Wanandoa maarufu nchini Marekani Julie na Todd Chrisley sasa wako huru kufuatia msamaha waliopatiwa na Rais Donald Trump.

Todd ndiye alitangulia kuondoka gereza la Pensacola, Florida saa chache baada ya Rais Trump kutia saini msamaha wao huku Julie akiondoka gereza la Lexington, Kentucky muda mfupi baadaye.

Wawili hao walipatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kulaghai benki na kukwepa kulipa ushuru ambapo walihukumiwa kifungo gerezani kila mmoja mwaka 2022.

Todd na Julie ambao ni wahusika hao wa vipindi vya runinga nchini Marekani walihukumiwa vifungo vya miaka 12 na 7 mtawalia gerezani kila mmoja lakini wamepata msamaha wa Rais baada ya kutumikia miaka miwili pekee.

Trump alitangaza msamaha wa wawili hao katika mawasiliano ya simu na binti yao Savannah Jumanne. Baada ya hapo Savannah aliandaa kikao na wanahabari kuwafahamisha kuhusu kuachiliwa kwa wazazi wake.

Mashabiki wa familia hiyo maarufu huenda wakafaidi kutokana na maelezo ya kina kuhusu kuachiliwa kwao katika kipindi kinachotarajiwa cha kuangazia maisha yao.

Huenda wasidaiwe tena dola milioni 17.8 zilizotokana na kesi dhidi yao.

Share This Article