Rais William Ruto anaongoza Maombi ya 22 ya Kitaifa yanayoendelea katika hoteli ya Safari Park, Jijini Nairobi.
Maombi hayo yaliyoandaliwa na Bunge la Kenya, yanahudhuriwa na wabunge wa Kitaifa, Senate na viongozi mbali mbali hapa nchini.
Wengine wanaohudhuria maombi hayo ni Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula, mwenzake wa Senate Amason Kingi pamoja na Mawaziri.
Huku Maudhui yakiwa “Inuka na Ujenge Upya”, maombi hayo yanapigia debe uwiano, Umoja wa Taifa na ugawanaji majukumu miongoni mwa viongozi.
Hafla hiyo ya kitaifa huwahimiza viongozi kutafakari kuhusu majukumu yao bila kujali miegemeo yao ya kisiasa, kidini na kuweka mbele maslahi ya taifa hili.