Watu 172 wafariki kutokana na kipindupindu Sudan

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 172 wafariki kutona na kipindupindu Sudan. Picha Hisani.

Ugonjwa wa kipindupindu umezuka nchini Sudan, na kusababisha vifo vya watu 172 na wengine zaidi ya 2,500 kuambukizwa katika muda wa wiki moja.

Kulingana na maafisa wa afya nchini humo, vituo vya afya vilivyoko vimeshindwa kumudu idadi kubwa ya wagonjwa wanaotafuta matibabu.

Ugonjwa huo umeripotiwa katika Jiji Kuu Khartoum, Omdurman, Kordofan Kaskazini, Sennar, Gazira, White Nile Mto Nile

Shirika la kimataifa la uokoaji IRC limetoa onyo kuhusu hali hiyo miaka mitatu tangu taifa hilo kutumbuia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Madaktari wamesema mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yameharibu umeme katika vituo vya kusafisha maji hivyo kulazimisha wengi kutumia maji yasiyo safi kwa kunywa.

Mkurugenzi wa shirika la IRC nchini humo Eatizaz Yousif, amesema vita vinavyoendelea vimechangia kuzuka upya kwa ugonjwa huo wakati usambazaji dawa na chanjo umedidimia.

Aidha upatikanaji wa huduma za matibabu umekuwa changamoto kubwa kwani wahudumu wa afya wamekimbilia usalama na wachache waliobaki hawawezi kukimu idadi ya wanaotafuta matibabu.

TAGGED:
Share This Article